Diamond Platnumz – Acha Nikae Kimya (Lyrics)

Mmm mmm
Mama ananambia Nassib mi ni mtu mzima na wee ndo nakutegemea
Yanayotokea jaribu kupiga kimya usidiriki ata kuongea
Mara nasikisikia vya aibu konda gwajima eti ugomvi umekolea
Kuchunguza karibu ni binti mmoja kwa mitandao wanachochea
Najariibu kunyamanza ila moyo hutakii
Unaniambia eti simba japo unguruma uisemee hakii
Ooh najaribu kunyamanza ata Laizer hataki yooh
Anasema walau nena kidogo hiih

Na mashabiki Dangote wananiambia mbona husemi chochote ah
Si uko nao siku zote ama ulezi unafanya uogope ah
Na media pande zote wanalalama kiongozi atoke eh
Nchi inaingia matope niende wapi na mi mtoto wa wote

Yani lawama wacha nikae kimya  nisiongee (Kimya)
Ooh ninyamanze mimi (Nikae kimya)
Nisiseme (Kimya) Mama kaniambia (Wacha nikae kimya)
Ooh nifunge mudomo (Kimya)
Mie bado mudogo sana (Nikae kimya) Nisiseme (Kimya)

Mmh ni mengi majaribu najitahidi epuka yasije nikost
Japo mengine swadakta mengine hayana maana
Rafiki kipenzi wa karibu hata nyimbo yake sikuweza ipost
Ila alivokamatwa iliniumiza sana
Mitandaoni kila kona uongo na ukweli unashonwa
Kila nyumba inanong’ona ah oh Tanzania
Mara kimbembe Dodoma bunge upinzani wamegoma
Juzi akapotea na Roma

Ohh Tanzania Ooh
Najaribu kunyamaza Makame hataki yooh ananiambia walau nena kidogo
Nyumbani nafungua gate niende kwa Mangi nunua spaghetti eh
Napewa za chini ya kapeti Kuna redio imevamiwa geti eh
Napita kwenye magazeti nakuta rundo la wetu Wameketi eh
Badala ya kutafuta senti wanabishana tu mambo ya vyeti

Wacha nikae kimya ooh nisiongee (Kimya)
Ninyamanze Kabisa (Nikae kimya) eh ulimi koma (Kimya)
Usije kunipoonza (wacha nikae kimya) nifunge bakuli langu (Kimya)
Nikojoe nikalale (Nikae kimya)
Mi bado mudogo sana (Kimya) Mama kaniambia

Oh najiuliza Waaaapi najiulii Waapi
Tunakwenda wapi Waapi kila siku maneno waaaa
Ah tuacheni jamani Waaapi mi na we ni taifa moja waaapi
Kambarage baba mmoja waaaa
Sa tofauti za nini tushikamane tukaijenge Tanzania

Related & Trending Posts
Loading...
Scroll Up